Monday, June 20, 2011

UTANDAWAZI NA MFUMO WA ELIMU TANZANIA

Mnamo miaka ya 1990 dunia ilishuhudia wimbi kubwa la utandwazi katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Utandawazi huu ulitokana na maendeleo makubwa ya viwanda na ushindani wa kibiashara hasa katika nchi za Ulaya.
Matumizi ya teknolojia katika sehemu mbalimbali kama vile viwandani, maofisini, hospitalini, taasisi za elimu na kwingineko yalikuwa kwa kasi, ikisaidia uzalishaji na utendaji kazi kwa wingi hasa katika nchi za ulaya huku nchi za Afrika zikibaki kuangalia matokeo ya utandwazi huo kama vile mashabiki wa mpira wa miguu.
Matokeo ya uzalishajh huu yalisababisha makampuni makubwa kuongezeka na mengine kuinuka kwa kasi. Kutokana hali hiyo ikasababisha sera ya uwekezaji katika Afrika kukua na sehemu nyingine kuundwa. Nch za Afrika zililazimika kuruhusu makampuni ya kigeni kuwekeza katika nchi zao bila masharti yoyote magumu.
Watanzania tulishuhudia makampuni ya kigeni yakiingia kwa kasi nchini baada ya sera ya utandawazi kupitishwa. Pia serikali ilidiriki kuuza mashirika ya umma kwa kisingizio cha uwekezaji ili kuongeza.
Swala likaja katika kuwapatia wananchi ajira katika makampuni hayo ya wawekezaji. Kigezo kimojawapo cha kupata ajira ni ufahamu wa lugha mbalimbali. Hii ni kwa sababu wawekezaji wametoka nchi nyngi kama vile Ujerumani, Uchina, India, Uingereza, Ufaransa, Marekani n.k.Watanzania wengi tunajivunia na Kiswahili na wachache kiingereza cha kuombea maji, hii ni kutokana na mfumo mbovu wa elimu.
Mfumo wa elimu ya Tanzania haujazingatia na wala sidhani kama unampango wa kuzingatia sera ya uwekezaji ili kuweza kuwaandaa wananchi katika soko la ajira katika ulimwengu huu wa utandawazi.
Mtoto ameanza shule ya msingi darasa la kwanza mpaka la saba, lugha ya kufundishiaa ni kiswahili. Akifika shule ya upili au sekondari lugha ya kufundishia inabadilika inakuwa kingereza, kuendelea mpaka chuoni. Msingi wa huyu mtoto ambaye anaandaliwa aingie kwenye soko la ushindani wa ajira ni mbovu. Huwezi kumfananisha na mtoto wa nch kama Kenya ambaye tangia darasa la awali anatumia kiingereza pamoja na lugha nyingine za kigeni. Hivyo soko la ajira lazima litushinde.
Baada ya Rwanda na Burundi kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchi ya Congo nayo iko mbioni kujiunga. Pia Sudan kusini. Lakini bado serikali inapiga porojo katika kuwaanda wananchi kuingia katika soko la ajira.
Nchi ya Rwanda imeingiza lugha mbalimbali katika mitaala yao mfano kichina. Hivyohivyo katika nchi ya Kenya.Hizi zote ni njia za kuwaandaa wananchi wao kukabiliana na ushindani wa ajira na biashara. Hapa kwetu lugha hizi zimebaki kufundishwa katika taasisi za utalii.Huku mitaala ikiboreshwa kila baada ya miaka kadhaa bila kuzingatia sera ya uwekezaji. Sasa unajiuliza wanavyokaa kuboresha mitaala hawa wanaojiita 'curriculum developers' wanaboresha nini, au wanajitengenezea mazingira ya kula posho zitokanazo na kodi za wananchi.
Bila mfumo wa elimu kubadilishwa na kuzingatia sera ya uwekezaji, wananchi wa Tanzania tutabaki kuwa walinzi katika mageti ya Wakurugenzi na Mameneja kutoka nchi za jirani.
Viongozi kazi yao ni kunenepesha matumbo yao kwa kutengeneza vikao visivyokuwa na msingi ili wapate posho zitokanazo na wavuja jasho pale Kariakoo.
Serikali kuu akiwemo Kiranja mkuu kuweni wazalendo tengenezeni mfumo wa elimu utakaotunufaisha.
Na sisi wananchi ukondoo umepitwa na wakati tuamke, tufanye mageuzi amani, amani, amani, wakati tunakufa maskini, wananeemeka wachache. Tafakari hili!.

No comments:

Post a Comment